Afisa wa Korea Kaskazini atorokea Korea Kusini

This is an image taken from video taken on April 5, 2004 of Thae Yong Ho, North Korean diplomat speaking during an interview in Pyongyang. North Korea diplomat Thae Yong Ho who was based in London has defected, according to South Korean officials.

Wizara ya muungano ya korea Kusini imeeleza kwamba afisa wa pili wa cheo cha juu katika ubalozi wa Korea Kaskazini mjini London amehamia Korea Kusini.

Msemaji wa wizara hiyo, Jeong Joon Hee, afisa huyo, Thae Yong Ho, akiandamana na familia yake, wamewasili katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul na wako chini ya hifadhi ya serekali.

Jeong aliwaambia maafisa wa serikali ya Korea Kusini kwamba alihama kwa sababu ya kuchukizwa na serikali ya Kim Jong Un wa Korea Kaskazini, na kuitamani demokrasia ya Korea Kusini pamoja pia na kujali mstakabal wa maisha ya watoto wake. Afisa huyo alikua katika ubalozi wa Pyongyang mjini London kwa miaka 10 akiwa na jukumu la kuimarisha sifa za nchi yake.