"Mimi binafsi nimeona jinsi matetemeko haya mengi yalivyosambaratisha vijiji, kuwahamisha maelfu ya watu na kuziacha familia nyingi zikihitaji msaada wa dharura wa kibinadamu na afya," alisema Alaa AbouZeid, kiongozi wa timu ya dharura ya afya ya WHO Afghanistan.
Akizungumza mjini Kabul Ijumaa, AbouZeid alisema, "Zaidi ya watu 114,000 wanahitaji msaada wa dharura wa afya ya kuokoa maish na kwamba madhara ya kiafya yaliyosababishwa na majanga hayo ni ya kushangaza."
Wale walioathiriwa zaidi na majanga hayo, alisema, ni wanawake, wasichana, wavulana na wazee, “ambao wanachangia zaidi ya asilimia 90 ya vifo na majeruhi, na kuongeza kwamba watoto wengi wameachwa yatima.”
Afisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu, au OCHA, inaripoti kwamba zaidi ya watu 66,000 wameathiriwa moja kwa moja na matetemeko ya ardhi, takriban 1,500 wameuawa, wengine 2,000 wamejeruhiwa, angalau nyumba 3,700 zimeharibiwa kabisa na majengo mengine 21,300 kuharibiwa kwa kiasi fulani.