Mashirika ya Afya yasaidia Afghanistan

Afghanistan yapatiwa chanjo ya polio.

Shirika la afya duniani, UNICEF na mashirika mengine Jumapili yameanza kuendesha chanjo ya polio nchini Afghanistan.

Shirika la afya duniani, shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine, Jumapili yameanza kuendesha chanjo ya polio huko Afghanistan, katika jimbo la kaskazini la Kunduz.

Kampeni ya siku tatu ya chanjo ya polio, inalenga kusitisha maambukizo yaliyo juu ya ugonjwa huo. Wataalamu wa masuala ya afya wanasema kesi mpya moja imeripotiwa huko Kunduz, lakini kama tatizo hilo halitazuiwa ugonjwa unaweza kusambaa haraka.