Afewerki: Eritrea haiungi mkono al-Shabab

  • Leylah Ndinda

Rais Isaias Afwerki, (kushoto), na rais Yoweri Museveni, (kulia), kwenye ikulu ya Entebbe, Uganda baada ya mkutano na waandishi habari, Thursday Aug.18, 2011

Rais wa Eritrea Isaias Afewerki amekanusha madai kuwa anaunga mkono na kufadhili kundi la wanamgambo wa al-Shabaab.

Rais wa Eritrea Isaias Afewerki amekanusha madai kuwa anaunga mkono na kufadhili kundi la wanamgambo wa al-Shabaab. Alisema madai hayo hayana ukweli huku akiwatolea changamoto wale wanaodai kuwa anaunga mkono Alshabaab watoe ushahidi.

Rais Isaias Afewerki alimaliza ziara ya nadra ya nchi ya kigeni huko Uganda kwa kukutana na rais Yoweri Museveni mjini Kampala, Alhamisi na kuzungumza juu ya masuala ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi zao mbili, mzozo wa Somalia, hali ya njaa pembe ya Afrika na masuala mengine ya bara la Afrika.

Katika mkutano wao wa pamoja na waandishi habari mjini Kampala Afewerki kwa kirefu alizungumzia kile alichokiita uvumi kuwa analifadhili kundi la wanamgambo la Al-shabaab.

Alisema madai hayo hayana ukweli huku akiwatolea changamoto wale wanaodai kuwa anaunga mkono Alshabaab watoe ushahidi.

Zaidi ya hayo kiongozi huyo wa Eritrea alikanusha madai kuwa ziara yake nchini Uganda ni kujaribu kutafuta uungaji mkono wa rais Museveni katika juhudi zake za kuirudisha nchi yake kwenye muungano wa IGAD na aondolewe vikwazo vya kuichumi ambavyo aliwekewa na Umoja wa Mataifa.

Rais Musreveni kwa upande wake alisema anamini kwamba Afewerki haungi mkono kundi la al-Shabab. Na aliongeza kusema kwamba kiongozi huyo amekubali kufanya kazi na nchi nyingine za kanda hiyo kutanzua mzozo wa Somalia.