AJALI YA MGODI TANZANIA

Ikiwa ni mwaka mmoja hivi leo tangu wananchi wa Tanzania kupoteza ndugu na jamaa zao katika migodi ya Mererani wilaya ya Simanjiro mkoani Arusha,jana wananchi wa Geita Magharibi mwa Tanzania nao walikumbwa na simanzi pale wachimbaji wadogo wadogo walipofukiwa katika migodi midogo midogo ya Geita.Inasadikiwa wachimbaji wadogo wadogo 36 huenda wamepoteza maisha katika migodi hiyo baada ya kufukiwa na vifusi kufuatia maporomoko ya mawe,miti na michanga.Khadija Riyami amezungumza na mzee wa kijiji huko Geita Ustaadh Thomas Makera ambaye anaishi kilometa chache kutoka kwenye migodi iliyokumbwa na ajali.