Ocampo aomba majaji kuiripoti Sudan

Ocampo aomba majaji kuiripoti Sudan

<!-- IMAGE -->

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu, Luis Moreno-Ocampo, amewaomba majaji kuiripoti Sudan kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuiheshimu hati za mahakama.

Mapema wiki hii, Moreno-Ocampo aliwaomba rasmi majaji kuwasilisha suala la kutopata ushirikiano kutoka serikali ya Sudan kwa kushindwa kumkabidhi waziri wa zamani wa masuala ya kibinadamu, Ahmed Harun na kiongozi wa wanamgambo Ali Kushayb.

Watu hao wawili walishtakiwa mwaka 2007 kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa vita nchini Sudan katika mkoa wenye mgogoro wa vita nchini sudan katika mkoa uliokumbwa na mzozo wa darfur.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir pia anatakiwa na mahakama hiyo kwa shutuma za uhalifu wa vita huko Darfur.