<!-- IMAGE -->
Akilihutubia taifa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru rais Abdoulaye Wade wa Senegal alisema taifa lake linachukua tena udhibiti wa makambi ya kijeshi yaliyokua yanashikiliwa na taifa la zamani la kikoloni la Ufaransa.
Rais Wade alisema makambi ya kijeshi ya Ufransa hayaambatani tena na uhuru wa taifa hilo la Afrika ya Magharibi. Alisema senegal inachukua udhibiti kuanzia usiku wa manane wa Jumapili. Tangazo hilo linafuatia makubaliano yaliyofikiwa mapema mwaka huu kati ya nchi hizo mbili ambapo Ufransa ilikubali kuwaondowa karibu wanajeshi wake 1 200 kutoka makabi yake Senegal.
Siku ya Jumamosi wakati a sherehe za uhuru rais Wade alizindua sanamu kubwa kabisa mjini mji mkuu wa Dakar. sanamu hilo lililogharimu dola milioni 20, llilopatiwa jina la Africa Renaissance, linalotaka kuonesha ufufuaji wa hali ya bara la Afrika, linasemekana kua refu kuliko sanamu zote barani humo.
Rais Wade, aliyesimamia mradi huo alisema Jumamosi kwamba sanamu linamulika malengo ya kaaida ya muafika ya kufanikiwa. wapinzani na wakosowaji wamelaani mradi huo wakiueleza ni uharibifu wa fedha katika nchi yenye watu wengi maskini na kwnda kinyuma na maadili ya kislamu.