Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan, amesema anasikitika kwamba serikali ya Kenya pamoja na bunge la taifa zimeshindwa kuunda mahakama nchini humo kusikiliza kesi za walohusika na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mwaka 2008.
Akiwahutubia waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake ya siku 3 mjini Nairobi, bwana Kofi Annan amesema kufikia mwishoni mwa mwezi huu majaji wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC huko The Haque, wanatarajiwa kutoa uamuzi wao ikiwa uchunguzi utaanzishwa rasmi dhidi ya washukiwa wa mauaji na ghasia hizo ambazo zilipelekea watu kukosa makazi.
Amesema kile anachoelewa ni kwamba majaji wanatoa uamuzi wao wiki ijayo na tutapata habari kamili juu ya nini kinachoendelea. Bwana Kofi Annan ambaye alitekeleza wajibu mkubwa kuwapatanisha viongozi wakuu nchini Kenya, Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga, punde tu baada ya uchaguzi huo uliokuwa na utata.