Kaimu Rais wa Nigeria ategemewa kukutana na Obama

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Nigeria amesema kaimu Rais GoodLuck Jonathan huenda akakutana na Rais wa Marekani Barack Obama mwezi ujao hapa Washington.

Mwanadiplomasia huyo wa zamani Ojo Maduekwe amesema Bw.Jonathan anapanga kusafiri kuja Marekani mwezi Aprili kuhudhuria mkutano kuhusu usambazaji nyuklia na huenda akapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na Obama.

Hii itakuwa ni safara ya kwanza kwa Bw.GoodLuck Jonathan nje ya nchi akiwa kama kiongozi wa nchi baada ya kuchukua madaraka ya uongozi kutoka kwa rais anayeugua Umaru Yar'Adua.