Wa-Iraki wapiga kura licha ya vitisho

Wa-Iraki walikaidi mashambulio ya mabomu na mizinga yaliyosababisha vifo vya watu 38 Jumapili na kupiga kura katika uchaguzi wa bunge unaochukuliwa ni mtihani mkubwa kwa demokrasia ya nchi hiyo.

Vituo vya kupiga kura vilifungwa magharibi na kura zimeanza kuhesabiwa, lakini Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba matokeo ya awali hayatapatikana mara moja bali baada ya siku kadhaa.

Waziri mkuu wa kishia Nouri al-Maliki, anakabiliwa na upinzani makubwa kutoka washirika wake wa zamani wa kishia pamoja na wanasiasa wa kisuni na kikurdi.

Hakuna chama kimoja kinatarajiwa kupata ushindi wa moja kwa moja, hivyo inaonekana serekali mpya itabidi kua ni ya mungano. Na yeyote atakaepata ushindi atasimamia kuondoka kwa majeshi ya marekani, mpango unaotazamiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.