Libya kuweka marufuku ya biashara dhidi ya Uswissi.

Serikali ya Libya imesema ina mpango wa kuweka marufuku ya biashara na uchumi kwa Uswissi.

Serikali ilitoa tangazo hilo Jumatano siku chache baada ya kiongozi wa Libya Muamar Gadaffi kutangaza Jihad au vita takatifu dhidi ya nchi hiyo ya Ulaya.

Gadafi wiki iliyopita aliwataka waislam kugomea bidhaa za Uswissi. Na kuishutumu Uswissi kuwa ni taifa la makafir kwasababu ya nchi hiyo imepiga marufuku ujenzi wa minara juu ya misikiti mingi.

Pia Jumatano Libya ilimshutumu msaidizi wa balozi wa Marekani na kutaka kuombwa radhi na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani P.J Crowley kuhusu wito wa Jihad wa Gadaffi.