Kamanda wa kijeshi wa kundi la waasi wanaotaka kujitenga katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabinda huko Angola amesema wapiganaji wake hawakuwa wanawalenga wachezaji wa timu ya taifa ya Togo walipofanya shambulio lao siku ya Ijuama.
Akizungumza na Sauti ya Amerikia idhaa ya Kireno, Kamanda Joao Batista, alisema wapiganaji wa FLEC walikua wanalenga kikosi cha jeshi la taifa la Angola na kwamba shambulio dhidi ya wachezaji ni matokeo ya ukosefu wa amani katika eneo hilo. Alitoa rambi rambi zake na kuomba samaha kutoka serekali ya Togo, akisema "hatuna chechote dhidi ya watu wa Togo au dhidi ya serekali ya Togo". Kamada huyo alisema kundi lake liko tayari kwa majadiliano na serekali lakini kuonya kwamba ikiwa serekali itakata pendekezo hilo basi kutakuwepo na mashambulio kama ilivyo kua awali. Waasi wa FLEC wamekua kwa miaka mingi wakipigania uhuru wa eneo hilo la Angola lenye utajiri mkubwa wa mafuta.Wakati huo huo timu ya kandanda ya Togo imeshaondoka Luanda kurudi nyumbani kufuatia shambulio hilo la Ijuma ambapo watu watatu waliuliwa. Wachezaji walieleza nia yao ya kubaki na kucheza katika finali za kombe la Afrika, lakini watalazimika kuheshimu mwito wa serekali ya kurudi nyumbani. Serekali ilipeleka ndege kuwarudisha wachezaji nyumbani.
Basi la timu ya wachezaji wa Togo lilishambuliwa siku ya Ijuma liulipokua linasafiri kupitia Jamhuri ya Kidemokrasia ya KOngoi kuelekea Cabinda, tayari kwuanza michuano siku ya Jumatatu.
Serekali ya Togo inaituhumu Angola kwa kutowaonya kuhusu ukosefu wa usalama huko Cabinda. Serekali ya Angola anasema timu ilikiuka masharti ya shirikisho la kandanda la Afrika CAF yanayohitaji timu zote kusafiri kwa ndege.