Wanaharakati wataka ufuatiliaji haki za binadam DRC

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imetolewa kwenye orodha ya kufuatiliwa na Umoja wa Mataifa tangu mwezi Machi mwaka 2008, ambapo wanachama 47 wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa walipokubali kuchukua uwamuzi huo kutokana na shinikizo kutoka nchi kadhaa.

Misri, nchi nyingine za kiarabu na za Afrika, na Russia zilikuwa miongoni mwa nchi zilizoongoza juhudi za kufukuzwa mtaalamu aliyechaguliwa kufuatilia hali ya haki za binadamu huko Congo.

Mkurugenzi mtendaji wa kundi la haki za binadamu, la UN Watch, Hillel Neuer, anasema hii ni mbinu ya kukejeli.

Anaiambia Sauti ya Amerika mgogoro wa Congo umeripotiwa kusababisha vifo vya watu wapatao milioni 5 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Anakiri kwamba wataalamu wa haki za binadamu hawawezi kusitisha ukiukaji mkubwa kama huo.

Neuer anasema hatua za baraza hilo juu ya Congo si ya kipekee, lakini sehemu ya mtindo unaojitokeza tangu baraza lilipoundwa mwaka 2006.