Wananchi wa Zimbabwe wamekuwa na maoni tofauti kufuatia matamshi ya Rais Robert Mugabe kuwataka wafuasi wake kujiandaa kwa uchaguzi ambao alisema utafanyika hivi karibuni.
Rais Mugabe alitoa matamshi hayo yenye nguvu kama kiongozi wa chama tawala cha Zimbabwe ZANU-PF, mwishoni mwa mkuu wa chama hicho.
Chama cha ZANU-PF kilipoteza viti vingi bungeni na kuchukuliwa na chama cha Movement for Democratic Change-MDC katika uchaguzi mkuu mwaka jana. Bwana Mugabe na kiongozi wa MDC, Morgan Tsvangirai baadae waliunda serikali ya umoja katika juhudi za kumaliza moja wa mgogoro wa kisiasa na uchumi.
Sauti ya Amerika imezungumza na mkazi wa mjini Harare, Melania Banga, kuhusu mtazamo uliopo kwa chama cha ZANU-PF.