Kombe la Dunia 2010

FIFA imepanga timu zote 32 katika makundi manane ya kuwania ubingwa wa kombe la dunia 2010 nchini Afrika Kusini, ambapo kundi la G limetajwa kuwa kundi la kifo kufuatia timu tatu zinazopewa nafasi ya kufanya vyema kupangwa katika kundi moja.

Timu hizo ni Brazil,Ureno, Ivory Coast na Korea Kaskazini ambayo inaonekana kuwa nyepesi katika kundi hilo.

Kundi C litakuwa na ushindani mkali kati ya Uingereza,Marekani, Algeria na Slovenia ambayo imeingia katika fainali hizo baada ya kuitoa Urusi.

Wenyeji Afrika Kusini wanaonekana kupumua kidogo licha ya kupangiwa Mexico, Uruguay na Ufaransa.

Makundi hayo ni kama ifuatavyo

Kundi A.
Afrika Kusini, Mexico, Uruguay na Ufaransa.
Kundi B.
Argentina, Nigeria, Korea Kusini na Ugiriki.
Kundi C.
England, Marekani, Algeria na Slovenia.
Kundi D.
Ujerumani, Australia, Serbia na Ghana.
Kundi E.
Uholanzi, Denmark, Japan na Cameroon.
Kundi F.
Italia, Paraguay, New Zealand na Slovakia.
Kundi G.
Brazil, Korea Kaskazini, Ivory Coast na Ureno.
Kundi H.
Uhispania, Uswisi, Honduras na Chile.


Akizungumza na Sauti ya Amerika kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Bw Sillersaid Mziray,anasema timu za Afrika zina nafasinzuri za kusonga mebeli kutokana na kupangwa katika makundi tofauti.

Mechi za ufunguzi kati ya Afrika Kusini na Mexiko inatarajiwa kufanyika June kumi na moja 2010.