Israel na Misri zatoa mwito wa amani

Viongozi wote wawili rais mkongwe wa Misri Hosni Mubarak, na mwanasiasa wa muda mrefu, rais wa Israel Shimon Peres, walitoa mwito wa kupatikana amani, na kusisitiza kwamba limebaki kua jambo linalowezekana, ingawa kumepaki masuala mengi yenye utata mkubwa. Marais wote walihimiza kuanza tena majadilano ya amani kwa haraka iwezekanavyo.

Bw. Mubarak alieleza kuwa nchi za Kiarabu zinaitaka Israel kusitisha ujenzi wote wa makazi ya walowezi, hasa huko Jerusalem, na kwamba mazungumzo lazima yanza kutoka mahala waliposita mwezi Mei mwaka jana.

Mubarak alisema kwamba, lazima amani iwapatiye wa- Palestine taifa huru, katika muda maalum ulopangwa na kuwa, nusu suluhisho au mipaka ya muda siyo jibu kamwe.

Rais wa Misri aliwahimiza viongozi wa Israel kuchukuwa hatua ya ujasiri ya kupatikana amani. Pia aliihimiza Israel kuondoa vikwazo dhidi ya Gaza, na kuondowa vizuwizi huko ukanda wa magharibi, na kuwaachia wapalestina kuweza kutembea kwa huru.

Rais wa Israel Shimon Peres, naye alimpongeza bw. Mubarak kwa jukumu lake la kuendelea na amani na kuheshimu mikataba kwa miaka 25. Bw. Peres alisema kuwa, vijana wengi wa kimisri wa kiisrael wanabidi kumshukuru kwa uwongozi wake na nia yake kwa ajili ya amani. Bw Peres pia alijibu ombi la bw Mubarak la kuitaka Israel kusitisha ujenzi wa makazi ya walowezi akisema.

“Tukiweza kuanza kwa haraka majadiliano, basi suala la makazi ya walowezi litaondoka, kwa sababu pale tutakapo kubaliana juu ya mipaka, hakutokuwa na matatizo, na itabidi kuyafikia kwa makubaliano. Tuko tayari kwa majadiliano, na tunatafuta suluhisho.”

Kiongozi wa Israel alisema Jerusalem sasa iko chini ya utawala wa Israel, lakini hata nayo pia huwenda ikawa sehemu ya makubalaino, iwapo itakubaliwa na pande zote.