Chanjo ya Malaria Yakaribia

Kampuni hiyo inasema kama majaribio yatafanikiwa kama ilivyopangwa, chanjo hiyo inaweza kusambazwa kwa Umoja wa Mataifa na vitengo vya madawa vya ulaya kuipitisha mwaka 2012. Rais wa kampuni hiyo, Jean Stephene, amesema kampuni ya GlaxoSmithKline, itafanya jitihada zote kuongeza upatikanaji wa chanjo hiyo.

Kampuni ya GlaxoSmithKline inasema chanjo hiyo ni ya kwanza iliyobuniwa kwa matumizi ya bara la Afrika, ambapo ugonjwa wa malaria unauwa zaidi ya watu laki nane kila mwaka, wengi wao wakiwa watoto. Kampuni ya kutengeneza madawa ya Uingereza hivi sasa inafanya majaribio ya mwisho ya chanjo hiyo. Utafiti utajumuisha watoto kumi na sita elfu kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Malawi, Msumbiji, Ghana, Gabon na Burkina.

Mkutano wa tano wa bara la Afrika juu ya Malaria unafanyika mjini Nairobi, ambapo wanasayansi, madaktari na wadau mbali mbali wanazungumzia chanjo hiyo mpya ya kupambana na malaria. Sauti ya Amerika imezungumza na Dr.Salim Abdullah kutoka Tanzania anayehudhuria mkutano huo.