Bomu la kando kando ya barabara lamwua afisa mwandamizi wa Somalia.

Maafisa wa ulinzi nchini somalia wamesema bomu la kutegwa kandokando ya barabara katika eneo lililojitenga limemuuwa afisa mwandamizi wa jeshi na watu wengine wawili.

Maafisa katika jimbo lililojitenga la Somaliland walisema jumapili kuwa bomu lililoteguliwa kutoka mbali lilimuua kamanda wa wanajeshi wa kitengo cha kinachofanya doria kwa miguu, osman yusuf.

Shambulizi lilifanyika katika mji wa lascanood ambalo yote Somaliland na Puntland yanadai ni la kwao.