Mjumbe maalum wa Marekani arudi Sudan kwa mazungumzo

Balozi Scott Gration anaelekea hadi Mjini Juba kituo cha kwanza cha ziara yake, ambako atakua na mazungumzo ya upatanishi kati ya wajumbe wa chama cha kaskazini cha National Congress, na kile cha kusini cha SPLM.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya juhudi za upatanishi za Marekani zilizoanza mwezi wa June. mwezi uliyopita mazungumzo hayo yalipelekea kutiwa saini hati inayo tanzua idadi fulani ya masuala yaliyokua yanakwamisha utekelezaji wa maubaliano ya amani ya 2005.

Mjumbe maalmu wa marekani baada ya hapo, atasafiri hadi Dafur kukutana na wawakilishi wa watu wa Darfur, ikiwa ni pamoja na wakazi wanaoishi katika kambi za walopoteza makazi yao, na viongozi wa makundi ya kiraia ya Darfur. Balozi Gration atakua pia na mazungumzo na kamanda mpya wa kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika, Jenerali Patrick Nyambumba kutoka Rwanda.

Kituo chake cha mwisho katika ziara hii itakua Khartoum ambako anapanga kukutana na tume ya Umoja wa Afrika inayoshughlikia suala la Darfur, inayongozwa na rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki. Tume hiyo maalum ya badhi ya viongozi wa zamani wa nchi za Afrika itatoa mapendekezo yake juu ya namna kutanzua mgogoro wa Darfur wiki ijayo.