LRA Yasababisha Wakimbizi DRC.

LRA Yasababisha Wakimbizi DRC.

Idara ya kuhudumia wakimbizi ya umoja wa mataifa inaripoti kuwa watu laki moja na elfu ishirini na tano kutoka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamelazimika kutoroka makwao baada ya kushambuliwa na kundi la waasi wa Uganda la Lord’s Resistance Army-LRA, katika muda wa wiki tatu zilizopita.

Shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa Mataifa linakubali kwamba watu laki moja na elfu ishirini na tano ni wengi mno kukimbia makwao katika muda wa majuma matatu. Kwa ujumla idadi ya watu waliotoroshwa makwao na waasi hao wa kundi la LRA katika wilaya ya Haute Uele katika jimbo la Orientale tangu mwezi Septemba mwaka jana ni zaidi ya milioni moja na nusu.

Msemaji wa shirika hilo Andrej Mahecic anasema idadi hiyo inaashiria ukatili unaotumiwa na waasi wa kundi la LRA.