Watoto wengi huko CAR wana utapiamlo

Idara ya kuhudumia watoto ya Umoja Mataifa inasema maelfu ya watoto katika Jamhuri ya Afrika ya kati wana utapiamlo wa juu. UNICEF inafanya utafiti wa hali ya utapiamlo huko CAR na katika matokeo ya awali kutoka majimbo matatu ya kusini magharibi mwa nchi umeonyesha kuwa zaidi ya watoto 16,700 au zaidi ya asilimia 220 wana utapiamlo mbaya sana. Idara hiyo imeomba msaada wa dola milioni moja na nusu ili kuwapatia chakula, madawa na vifaa vingine watoto katika muda wa miezi sita ijayo.