Mafua ya nguruwe yaingia Kenya

Wanafunzi wasiopungua 34 kutoka chuo kikuu cha Notingham nchini Uingereza wametakiwa na serikali ya Kenya kuondoka nchini humo baada ya baadhi yao kukutwa na virusi vinavyosababisha mafua ya nguruwe. Hii ni mara ya kwanza kwa ugonjwa huo kugundulika nchini humo tangu utokee nchini Mexico. Serikali ya kenya imetangaza Jumatatu kuwa watu wapatao 20 wamepatikana na ugonjwa huo hasa katika mji wa Kisumu na mkoa wa kaskazini mashariki.

Taarifa zaidi zinasema wanafunzi hao wameondoka nchini Kenya pole pole baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina na maafisa wa afya katika hoteli walimokuwa wakiishi mjini Kisumu ambapo walikaa mjini humo kwa muda wa siku kumi na moja.

Wanafunzi hao waliwasili nchini Kenya kwa shughuli mbali mbali ikiwa ni pamoja na kazi ya kujitolea.