Rais Kikwete atangaza mpango wa kufufua uchumi

Akiwahutubia wabunge na wazee huko bungeni Dodoma siku ya Jumatano, Rais Jakaya Kikwete alisema serekali itahakikisha kutoa mikopo kwa makampuni katika sekta za utali, kilimo na sekta nyenginezo, na kulipa fidia baadhi ya makampuni yaliyopatwa na hasara kubwa moja kwa moja.

Kiongozi huyo wa Tanzania alikua anazungumza kabla ya kutangazwa bajeti ya taifa kwa mwaka 2008/09. Alisema serekali itazilipa benki zilizokopesha kampuni hizo moja kwa moja, lakini hawatoilipa madeni ya zamani yasiyohusiana na mzozo wa hivi sasa.

Rais Kikwete alisema mpango wa pili ni kuhakikisha ratiba ya malipo madeni yanajadiliwa upya kwa makampuni yaliyo athirika hasa viwanda, utali na kilimo.

Mhadhiri wa masuala ya kisiasa Bashir Ally ameiambia Sauti ya Amerika anasema inabidi kukubaliana kwamba mzozo huu wa uchumi unaoikumba Tanzania hautokani hasa na mzozo wa uchumi duniani bali pia kutokana na sera mbaya zinazotumiwa tangu miaka ya 1980 ya kurekebisha uchumi.

Anasema ana wasi wasi, ikiwa mpango wa kunusuru uchumi hauta angalia upya sera za nchi hiyo, basi hadhani wataweza kunusuru uchumi kwa mpango wa miaka miwili wakati uchumi umeathirika kwa miaka zaidi ya 20 iliyopita.