UN Kujishughulisha Zaidi na Migogoro ya Afrika

Wakati wa ziara yao Jumapili kwenye makumbusho ya mauwaji ya kimbari ya Rwanda, wajumbe wa Baraza la Usalama walikumbushwa moja ya mambo makubwa ambayo Umoja wa Mataifa ulishindwa kutekeleza.

Kiongozi mkuu wa makumbusho Honore Gatera aliwambia wajumbe hao jinsi Umoja wa Mataifa ulivyoondoa wanajeshi wake licha ya kujua fika hatari iliyokuwa inaikabili nchi ya Rwanda.

Jumamosi wajumbe wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Mataifa walikuwa mjini Addis Ababa kuzungumzia machafuko yanayoendelea Somalia. Wajumbe hao wa UN waliwaambia wenzao wa AUkuwa Umoja wa Mataifa utachukua jukumu la kulinda amani nchini Somalia.