Annan kuwasilisha majina ya wa Kenya huko The Hague

Katibu Mkuu wazamani wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan, amesema atawasilisha bahasa yeneye majini ya walohusika na ghasia zilizosababisha mauwaji huko Kenya mapema mwaka 2008, ikiwa serekali ya nchi hiyo haitounda mahakama maalum kusikiliza kesi zao. Bw Annan alikua anazungumza mjini Geneva baada ya mkutano wa siku mbili ulojadili mafanikiyo na changamoto zinzokabili utawala wa mseto huko Kenya.

Kufuatia onyo hilo la Katibu Mkuu wa zamani, Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu ICC huko The Hague Uholanzi, imeonya kwamba iko tayari kuchukua hatua ikiwa serekali ya Kenya haitofanya lolote kuwahukumu walohusika na njama za ghasia zilizosababisha mauwaji ya karibu watu 1 500 na maelfu kujeruhiwa na maelfu wengine kupotezamakazi yao.Mwandishi wa kiuto cha televisheni ya Kenya KTN, Kai Kai aliyehudhuria mazungumzo anasema hakuna matokeo muhimu yaliyofikiwa lakini mkutano ulikua hatua muhimu wa kutathmini mafanikio na matatizo ya utawala wa kugawanya madaraka huko Kenya.