Mawaziri 7 wa Kenya Marufuku Kuingia Marekani

  • Mwai Gikonyo

Hii ni mara ya pili kwa serikali ya Marekani kuwapiga marufuku mawaziri saba wa Kenya kuingia Marekani, kwa madai kuwa walihusika na rushwa au machafuko yaliyofuatia uchaguzi wa rais nchini Kenya, uliofanyika Disemba 2007.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Michael Rudenburg anasema waziri ambaye amepigwa marufuku na serikali ya Marekani, amekuwa akijihusisha na rushwa kwa muda mrefu. Lakini Balozi Rusengurg amekataa kutaja jina la waziri huyo.

Balozi huyo amesema serikali ya Marekani ina haki kamili ya kusimamisha hati ya kusafiria ya mtu yeyote anayejihusisha na rushwa au kunufaika kwa namna moja au nyingine na vitendo vya rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma.

Lakini Waziri wa Kilimo wa Kenya, William Rutto ambaye hivi karibuni alikabiliwa na shutuma kali kutoka kwa wabunge na wananchi wa kawaida, amesema kila nchi inahaki ya kumzuwia mtu yeyote ambaye hawataki aingie nchini mwao.