Obama ahimiza mpango wa kuufufua uchumi

Rais Barack Obama anafanya kila jitihada kuhakikisha bunge la marekani linaidhinsha mpango wake wa kuufufua uchumi na akadokeza uwezekano wa baadae kwa kua na mazungumzo ya moja kwa moja na iran. Alizungumzia masuala hayo mawili alipokutana kwa mara ya kwanza jumatatu usiku na waandishi habari wa ikulu.

Rais aliuitisha mkutano huo na waandishi habari na kuonekana kote nchini katika juhudi zake za kupata uungaji mkono mkubwa kabisa kwa mpango wake unaojadiliwea bungeni kwa wakati huu. Alisema " Almuradi, wakati wote nitakapo shikilia uwongozi wa afisi hii nitafanya kila inayohitajika kuufufua tena uchumi na kurudisha nchi kufanya kazi"

Alisema wakati sekta ya binafsi imevunjika nguvu kutokana na kuduma kwa uchumi ni lazima kwa serekali kuingilia kati kusaidia. Alisema usipofanya chechote kwa hali mbaya kama hii ya uchumi basi unazorotesha zaidi mambo na kusababisha kua vigumu kujikomboa kutokana na mgogoro huo alisema rais Obama.

Ingawa masuala mengi yalihusiana na uchumi lakini Rais Obama alizungumzia masuala ya kigeni, akisema kuna ishara za mawasiliano ya kidiplomasia yatanza na anasema katika miezi inayokuja huwenda kukatokea nafasi ya kukaa kwenye meza moja, ana kwa ana kwa mazungumzo ya kidiplomasia na Iran.

Kuhusu Afghanistan, Rais Obama alisisitiza wasi wasi wa kutokuwepo na maendeleo ya kisiasa ikiwa nyuma ya Iraq. Alisisitiza kwamba serekali ya washington inatathmini hivi sasa sera ya Washington kuelekea Kabul.