Maandamano makubwa yamefanyika mashariki ya kati na sehemu nyingine duniani, kupinga mashambulio ya mabomu yanayofanywa na Israel katika eneo linalodhibitiwa na Hamas la Ukanda wa Gaza.
Maelfu ya wapalestina wanaoishi Ramallah, walinyoosha juu mabango na kutamka maneno ya umoja, wakiungana na wapalestina wenzao huko Gaza, huku majeshi ya Israel yakiwa yamewekwa katika hali ya tahadhari kubwa.
Nchini Kenya baadhi ya makundi ya waislam yamepeleka malalamiko yao katika ubalozi wa Israel kupinga mashambulio ya Israel dhidi ya wapalestina Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao wamesema kuwa vita inayofanywa Ukanda wa Gaza inaathiri hali ya kibinadamu kwa wapalestina, ambapo watoto na wanawake wanateseka na wengine kuuwawa.
Makundi hayo ya kiislam yaliyokuwa yamebeba mabango ya kuikashfu Israel, yamesema kuwa balozi wa Israel nchini Kenya anastahili kufukuzwa, kwa maelezo kuwa nchi yake yaijali haki za binadamu.