Miaka 60 ya Mkataba wa Haki za Binadam

Watu wengi duniani wanachukulia hii leo kwamba kuwepo na haki za binadam ni chombo muhimu cha jamii iliyostarabika. Lakini larry cox wa Amnesty International, AI kitengo cha Marekani anasema mkataba wa haki za binadam ni matokeo ya wakati muhimu kabisa ya historia duniani.

Anasema, "unatokana na mateso na maovu ya vita vya pili, kipindi cha kuduma uchumi duniani na mauwaji ya wayahudi, holocaust, mambo hayo yakaifanya dunia kutambua kuna haja ya hatua kuchukuliwa.

Umoja wa Matiafa hatimae ukapitisha mkataba kwa kura 48 bila ya kupingwa, na ikabidi kuchukuliwe hatua kubwa za kidiplomasia kuyarai mataifa mengine duniani kukubaliana na mkataba huo.

Bi Mariam Kahiga mkurugenzi wa AI huko Kenya anasema mkataba huo umeleta manufaa chungu nzima kwa Afrika. Anasema jambo moja kuu ni kuyasaidia mataifa kupanga na kupitisha sheria za kitaifa za haki za binadam