Maharamia wa panga njama zao Mombasa

Tangu maharamia kuanza kuteka nyara meli kubwa kubwa mapema mwaka huu na kudai fidia za mamilioni ya dola kila mtu amekua akiuliza imekuaje kwa maharamia hao kua ujabari kama huo? Na jee ni nani wanao waongoza au kuwatuma? Waatalamu na wachambuzi wanasema yote haya yanatokana na ukosevu wa utulivu huko Somalia, na sas mapigano ya ardhini yameenea baharini.

Lakini tangu Marekani, Umoja wa Uaya na nchi nyenginezo kupeleka manuari za kijeshi kulinda eneo hilo kubwa la bahari ya Hindi, kumeanza kutokea fununu kwamba kuna watu njee ya Somalia wanaohusika. Mkuu wa shirika la wanabaharia huko Mombasa Andrew Mwangura anasema wakuu wa usalama wanafahamu kabisa juu ya shughuli za watu hao na wanashanga kwanini hakuna wanaokamatwa.

Mwandishi wetu huko Mombasa Abdulsalam Hamid anasema wakuu wa usalama wanasema ni mtandao mkubwa na upelelezi unaendelea na hivyo hawako tayari kutaja majini baado.

Wachambuzi wanasema mkwa vile meli ya mwisho ambayo ni kubwa sana ya kifahari ya kitali Nautica kushambuliwa na kukimbia huwenda usalama ukaimarishwa. Mashirika mengi ya meli hivi sasa yanasema yataweka maafisa wa usalama katika meli zinazopita katika huko ghuba ya aden.

Lakini wachambuzi wengi wanasema njia pekee ni kupatikana utulivu na serekali ya kudumu huko Somalia, kabla kuweza kumaliza tatizo hilo uharamia.