Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema bei za juu za vyakula, kiangazi na mizozo katika baadhi ya maeneo ya ulimwengu vinaendelea kuchangia kuongezeka kwa njaa.
WFP inakadiria kuwa watu milioni 17 katika pembe ya Afrika wanahitaji msaada wa chakula, huku mamiliioni wakiendelea kuathiriwa na kiwango cha juu cha utapia mlo.
Wataalamu wa misaada wanashirikiana kuhakikisha utapia mlo na vifo vya watoto wachanga havifikii viwango sawa na ukame.
Programu ya chakula duniani inakabiliwa na wakati mgumu kupata wasafirishaji wa kupeleka chakula katika bandari za Somalia, na katika kipindi cha mwaka mmoja baadhi ya sehemu za Somalia zinazorota na kuingia katika hali ya ukame.