Gavana Paluku tayari kuzungumza na Nkunda

Katika juhudi za kutafuta amani huko kaskazini mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, gavana wa jimbo la Kivu ya kaskazini amesema yuko tayari kua na mazungumzo ya ana kwa ana na kiongozi wa waasi Jenerali Laurent nkunda.

Gavana Julien Paluku akizungumza na Sauti ya Amerika anasema msimamo huo wake hautafautiani na ule wa serekali ya Kinshasa. Amesema akiwa mkuu wa jimbo yeye ni mwakilishi wa serekali na kwa vile yeye ni kiongozi aliyechaguliwa na wananchi, ni jukumu lake kuhakikisha wanaishi kwa amani.


Paluku anasema ni muhimu kwake kuzungumza na Nkunda kujua ni nini hasa anachokitaka na kwanini anaendelea kupigana, ikiwa ni kwa lengo la kuwalinda watu wa kabila lake la Watutsi basi mazungumzo ndiyo njia pekee kufuatana na makubaliano ya amani ya Goma.