Wabunge Kenya Wakataa Ripoti ya Jaji Philip

  • Mkamiti Kibayasi

Wabunge wa chama cha ODM nchini Kenya wameikataa ripoti ya jaji Philip Waki wa Afrika Kusini, iliyochunguza watu wanaodhaniwa kuhusika na ghasia zilizofuatia uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka uliopita.

Mmoja wa wabunge kutoka chama cha ODM, mheshimiwa Ababu Namwamba amesema ODM imechukua msimamo huo kutokana na dosari zilizokkuwepo katika ripoti hiyo ambazo zinafanya utekelezaji wake kuzua vurugu nchini humo na kutotenda haki kwa wahusika.

Wabunge hao wamependekeza zitafutwe njia nyingine ambazo zinaweza kutumika ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wale wanaodhaniwa kuhusika na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu.