Serikali ya Tanzania Yashutumiwa Kufanya Ubabe

  • Marry Mgawe

Serikali ya Tanzania imewapiga marufuku wazee wastaafu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya mikusanyiko au mikutano ya aina yoyote nchini humo kwa kwa madai kuwa ni kinyume cha sheria.

Msemaji wa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki Manase Mlaki amesema leo Jumatatu kuwa kuwa amepata barua kutoka jeshi la polisi la nchi hiyo, likiwataka kuacha mikutano ya madai ya malimbikizo ya marupurupu, kwa madai kuwa wafanyakazi hao walikuwa vibarua na hawastahili kupewa malipo.

Juhudi zao za kutaka kumwona rais Jakaya Kikwete wa Tanzania kwa lengo la kutatua mzozo huo zimegonga mwamba na badala yake wameishia kupewa vitisho.

Mwezi uliopita maelfu ya wastaasfu hao waliandamana katika maeneo ya jiji la Dar es Salaam, wakielekea ubalozi wa uingereza, nchi ambayo iliingia mkataba na serikali ya Tanzania kuwalipa wazee wao.

Aidha bwana Manase amesema Novemba 4 mahakama kuu ya Tanzania ilitoa maelezo ya kulipwa wazee hao wa Jumuiya ya Afrika mashariki kwa kuzingatia vipengele 14 vilivyomo katika madai yao.