Ruhusa ya kamari mitandaoni yazua hofu ya uhalifu Thailand

Mipango ya Thailand ya kuhalalisha uchezaji kamari mtandaoni inazua hofu kwamba magenge ya wahalifu yatatumia mwanya huo kuhamisha na kutakatisha fedha haramu kama walivyofanya na waendeshaji kamari katika nchi jirani.

Prasert Jantararuangtong, waziri wa uchumi wa kidijitali wa Thailand na jamii, amesema wiki iliyopita kwamba muswada unaweza kuwa tayari ndani ya mwezi mmoja.

Waziri Mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra, ambaye anaonekana kuwa na nguvu kubwa nyuma ya serikali ya sasa, inayoongozwa na bintiye Paetongtarn Shinawatra, aliidhinisha wazo hilo pia wiki iliyopita.

Msukumo uliozuiliwa wa kushinikiza umekuwa wa kiuchumi na kisheria.

Thaksin alidai sekta ya kamari ya mtandaoni inayodhibitiwa inaweza kuipatia serikali karibu dola bilioni 3 ya mapato ya kila mwaka.

Kwa kufanya uamuzi huo utaiweka sekta wazi, Prasert amesema hatua hiyo inaweza pia kuwafukuza wahalifu walio nyuma ya tovuti nyingi za kamari.