Maelfu ya watu waandamana kabla ya kuapishwa kwa Trump

  • Abdushakur Aboud

Maelfu ya watu wahudhurua mkutano wa People's March Washington

Maelfu ya watu wengi wao wanawake waliandamana mjini Washington Jumamosi Disemba 18, 2025, kulalamika dhidi ya kuapishwa kwa rais mteule Donald Trump, na kutoa ujumbe wa kulinda haki zote za kiraia na kibinadamu.

Maandamano yaliyopewa jina la "People's March" yalianza kutoka uwanja wa Franklin na kupita kati kati ya jiji la Washington hadi uwanja mkubwa mbele ya makumbusho ya Lincon.

Maandamano ya "People's March" kabla ya kuapishwa Trump

Waandamanaji walikusanyika pamoja na kusikiliza hotuba kutoka viongozi wa asasi mbali mbaloi za kiraia kuhusiana na kulinda demokrasia, haki za wanawake hadi haki za uzazi na usawa wa kijinsia na haki za mashoga.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Analilia Mejia, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Popular Democracy, amesema maandamano hayo yana lengo la kuwaleta pamoja wanaharakati na waungaji mkono ili kuwakumbusha masuala muhimu ya demokrasia yanayokabiliwa na kitisho chini ya utawala mpya.

Maandamano ya People's March yaanza kutoka uwanja wa Farragut, Washington

Anasema ujumbe muhimu ni kuhakikisha vita vinaendelea na mageuzi ya kweli yanapatikana baada ya vita vya muda mrefu.

Maandamano ya mwaka huu yakupinga kuapishwa kwa Trump yamekua madogo zaidi kuliko myale yaliyofanyika wakati wa awamu yake ya kwanza 2017, kwa sehemu fulani ni kutokana na vuguvugu la kutetea haki za wanawake Marekani limegawika baada ya Trump kumshinda makamu rais Kamala Harris mwezi Novemba.

Maandamano ya People's March Washington DC, 2025

Trump aliwasili Washington Jumamosi na ameanda karamu katika klabu yake ya mchezo wa Golf mjini Sterling, Virginia na atahudhuria mkutano wa ushindi wake katika uwanja wa Capitol One Arena, Washington siku ya Jumapili ulopewa jina la "Make Amerika Great Again".