Viongozi wa dunia kwa upande wao wamekua wakipongeza makubaliano hayo yaliyotangazwa na waziri mkuu wa Qatar, Sheikh Mohammed Bin Abdulrahman al-Thani siku ya Juamtano Januari 15, 2025.
Al-Thani anasema, makubaliano yanaeleza kwa makini juu ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya wiki sita, inayohusisha kuondoka kwa utaratibu wanajeshi wa Israel kutoka Gaza na kuachiliwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas kwa kubadilishana na wafungwa wa Palestina wanaoshikiliwa na Israel.
Makubaliano yamefikiwa miezi 15 baada ya wapiganaji wa Hamas kuishambulia Israel Oktoba 7, 2023, na kuwauwa wa Israeli 1,200 na kuwateka nyara raia 250 wa kigeni na Israeli.
Shambulio hilo lilipelekea mapigano yaliyosababisha vifo vya maelfu ya wapalestina, uharibifu wa Gaza na kuzusha mvutano huko Mashariki ya Kati.
Rais Joe Biden wa Marekani amepongeza matokeo hayo aliyoeleza yamepatikana baada ya majadiliano magumu kabisa ambayo hajawahi kushuhudia katika maisha yake ya kisiasa.
Amesema "ilikua ni kushindwa kwa siku 700 na siku moja ya mafanikio. Tumekua na siku nyingi za hali ngumu tangu Hamas kuanzisha vita hivi vibaya."
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akipongeza makubaliano amesema kipaumbele kina bidi kuwa kupunguza maadhila ya watu wa Gaza akionya kwamba usalama unaweeza kuzusha hatari katika kuwasilisha msaada wa dharura.