Huenda zaidi ya watoto 3,000 kutoka makabila ya jadi ya Marekani walikufa kwenye shule za bweni-Washington Post yasema

  • VOA News

Watu wa makabila ya jadi wa Marekani kwenye jimbo la Arizona

Huenda takriban watoto 3,104 kutoka makabila ya jadi walikufa kwenye shule za bweni Marekani baada ya kuondolewa kutoka kwenye familia zao kwa nguvu wakilazimishwa kuingia kwenye mfumo wa kawaida wa maisha, gazeti la The Washington Post limeripoti Jumapili.

Kwenye shule hizo ambazo baadhi zilikuwa za kidini kuanzia mwanzo wa karne ya 19 hadi miaka ya 70, watoto wengi walipitia unyanyasaji wa kimwili, kisaikolojia pamoja na kijisnia, kulingana na ripoti ya serikali ya hivi karibuni, iliyokisia kuwa takriban wanafunzi 973 walikufa. Mwishoni mwa Oktoba, Rais wa Marekani Joe Biden aliomba msamaha kutoka kwa watu wa makabila ya jadi ya Marekani, akisema kuwa ukatili huo, “ni donda linalotia mawaa myoyo yetu.”

Kulingana na The Washington Post iliyofanya uchunguzi kwa mwaka mmoja, wanafunzi 3,104 walipoteza maisha yao kwenye shule hizo kati ya 1828 na 1970, kwa kile kimeelezwa na gazeti hilo kama kipindi cha giza katika historia ya Marekani na ambazo kimepuuziwa na kufichwa sana. Washington Post imeendelea kusema kuwa imedhibitisha kuwa zaidi ya wanafunzia 800 miongioni mwao walizikwa kwenye makaburi yaliokuwa karibu na shule zao, na kwamba mara nyingi miili ya watoto hao haikurejeswa kwa familia wala makabila yao.