Takriban watu 18 walifariki dunia wakati boti iliyokuwa imebeba abiria ilikuwa inaelekea sokoni katika mkoa wa Far North nchini Cameroon ilipopinduka, afisa utawala wa eneo hilo alisema Ijumaa.
Ajali hiyo ilitokea siku ya Alhamisi kwenye maji kuelelekea wilaya ya Darak, kisiwa kilicho katika Bonde la Ziwa Chad karibu na mpaka wa Chad, ambako mafuriko ya msimu yamefanya boti kuwa njia pekee ya kuzunguka katika eneo hilo.
Mamat Zarma, afisa tarafa ya Darak, alisema boti hiyo ya mbao ilikuwa njiani wakati ilipotikiswa na upepo mkali, na kusababisha kupinduka.
Wiki mbili zilizopita, tukio kama hilo lilitokea katika wilaya ya karibu ya Goulfey, wakati mtumbwi uliotenegenezwa kienyeji uliokuwa na abiria 30 ulipopinduka, na kuua watu wanne na wengine kadhaa kupotea.