Rais Samia ataka uchunguzi wa kina kufuatia kifo cha afisa wa Chadema

Samia Suluhu Hassan akihuduria mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Bejing

Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ametowa salamu za rambi rambi kwa viongozi wa chama cha upinzani cha Chadema na familia ya Ali Mohamed Kibao kufuatia kifo cha afisa huyo muandamizi.

Rais Samia ametoa salamu hizo siku ya Jumapili Septemba 8, 2024 kupitia ukurasa wake wa mtandao.

Kiongozi huyo ameandika kwamba, amepokea kwa usikitifu mkubwa kifo cha kiongozi huyo wa Chadema na kutaka uchunguzi wa kina na haraka ufanyike.

"Nimeagizia vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumili vitendo vya kikatili vya namna hii," ameandika Rais Samia.

Maafisa wa chama wanasema, Kibao ambae ni mjumbe wa Baraza Kuu la Kitaifa la Chadema, alishushwa kwa nguvu kutoka basi la Tashrif na watu waloikua na bunduki siku ya Ijumaa Septembe 6, 2024 alipokua anasafiri kutoka Dar Es Salaam kuelekea Tanga.

Ali Mohamed Kibao, afisa muandamizi wa Cahdema Tanzaniua

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi la Polisi, David Misime inaeleza kwamba uchunguzi unafanyika baada ya kupata taarifa kutoka katibu mkuu wa chama cha Chadema John Mnyika na vyombo vya habari.

Mwili wa Kibao unasemekana uligunduliwa Jumamosi usiku katika chumba cha maiti mjini Dar es Saalam.

Tukio hilo limetokea chini ya mwezi mmoja baada ya Mbowe, naibu wake Tundu Lissu na viongozi wengine wa Chadema kushikiliwa kwa muda kufuatia kukamatwa watu kabla ya kufanyika mkusanyiko wa vijana wa chama hicho.