Nigeria imeipiga faini kampuni ya Meta ya dola milioni 220 ambayo ni kampuni mama ya Facebook na WhatsApp, kwa ukiukaji wa mara nyingi na unaojirudia
Nigeria imeipiga faini kampuni ya Meta ya dola milioni 220 ambayo ni kampuni mama ya Facebook na WhatsApp, kwa ukiukaji wa mara nyingi na unaojirudia.
Tume ya serikali kuu ya Ushindani na Ulinzi wa Wateja (FCCPC) siku ya Ijumaa iliishutumu Meta kwa kukiuka ulinzi wa data wa nchi na sheria za haki za watumiaji kwenye mtandao wa Facebook na WhatsApp.
Afisa mkuu mtendaji wa FCCPC Adamu Abdullahi alisema uchunguzi uliofanywa na tume hiyo kwa kushirikiana na Tume ya Kulinda Data ya Nigeria kati ya Mei 2021 na Desemba 2023 ulionyesha kuwa ilijihusisha na vitendo vya kuingilia watu au watumiaji wa data nchini Nigeria.