Waziri Mkuu wa China, Li Qiang, Jumapili amempongeza Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Keir Starmer kwa kuchaguliwa kwake, vyombo vya habari vya serikali vimeripoti akiwa ni kiongozi mkuu wa kwanza wa Beijing kufanya hivyo hadharani.
China “iko tayari kufanya kazi na serikali mpya ya Uingereza ili kujumuisha uaminifu wa kisiasa na kupanua ushirikiano wenye mafanikio,” Li alimueleza Starmer, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua.
Wito wao umetolewa baada ya siku kadhaa za ukimya kutoka kwa maafisa wakuu wa Beijing, huku wizara ya mambo ya nje ya China ikisema ilifahamu matokeo ya uchaguzi wa Uingereza muda si mrefu.
Kwa kulinganisha, kiongozi wa China Xi Jinping alimpongeza Rais mpya wa Iran, Masoud Pezeshkian saa chache baada ya kuchaguliwa wake Jumamosi.