Ndege aina ya Boeing 737 iliyokuwa imebeba watu 85 ilipata ajali kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Dakar, mji mkuu wa Senegal, na kuwajeruhi watu 10, waziri wa uchukuzi amesema leo Alhamisi.
Waziri wa uchukuzi wa Senegal, El Malick Ndiaye amesema ndege hiyo ya Air Sénégal inayoendeshwa na TransAir ilikuwa ikielekea Bamako Jumatano jioni ikiwa na abiria 79, marubani wawili na wafanyakazi wanne wa ndege. Waliojeruhiwa walipatiwa matibabu katika hospitali moja ya eneo huku wengine wakipelekwa hotelini kupumzika.
Hakuna maelezo zaidi yaliyopatikana mara moja. Mtandao wa Usalama wa Anga, ambao unafuatilia ajali za ndege, ulichapisha picha za ndege hiyo kwenye mtandao wa X zamani ikijulikana Twitter, ikionyesha ndege ikiendelea kusaidiwa na huduma za kikosi cha zimamoto.
Injini moja ilionekana kuwa imevunjika na bawa pia liliharibiwa, kulingana na picha hizo. ASN ni sehemu ya taasisi ya Usalama wa Ndege, shirika lisilo la kiserikali ambalo linalenga kuboresha usafiri salama wa anga na kufuatilia ajali.