Mahakama ya Katiba nchini Mali imejitangaza yenyewe kuwa haina uwezo kuchunguza kesi inayotaka utawala wa kijeshi kusitisha shughuli za vyama vya kisiasa kubatilishwa.
Katika waraka ulioonekana na shirika la habari la AFP leo Jumamosi, mahakama hiyo pia ilitoa uamuzi wa kutoruhusiwa ombi kutoka kwa vyama vya mahakimu na waendesha mashtaka, kuiona kuwa Mali ilikuwa na mapungufu ya kisheria au mwanya wa kitaasisi na kupanga mchakato wa kurejea katika uchaguzi. Hukumu zote mbili za mahakama zilitolewa siku ya Alhamisi.
Taifa hilo la Afrika Magharibi limetawaliwa na serikali ya kijeshi tangu mapinduzi ya mwaka 2020 na 2021, huku hali ya usalama ikizidi kuzorota kutokana na makundi ya wanajihadi na wanaotaka kujitenga.