Kati yao ni msemaji wa kundi la M23 Meja Willy Ngoma.
Wengine ni viongozi wa kundi la Allied democratic forces na FDLR wakiwiemo Apollinaire Hakizimana, Ahmad Mamood, Mikel Rukunda, Mohamed Ali Nkalubo, na William Amuri.
Vikwazo vinawazuia kupata silha, mafunzo, msaada wa kifedha na kusafiri
Taarifa ya baraza la usalama la umoja wa mataifa inasema kwamba Ngoma amelengwa kwa kuwa mmoja wa viongozi wa kisiasa na kijeshi wa kundi la waasi la M23 linaloshutumiwa kwa vita, mauaji na mateso ya raia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Waasi wa M23 wanaoripotiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa DRC wakitaka kudhibithi mji wa Sake karibu na Goma.
Marekani ilimuwekea vikwazo Meja Willy Ngoma mnamo mwezi Desemba mwaka 2023 kutokana na mashambulizi na mauaji ya raia mashariki mwa Jmahuri ya kidemokrasia ya Congo.