Watu kote nchini Haiti wanashangaa nini kitatokea baada ya mahakama nchini Kenya kuzuia kupelekwa kwa kikosi cha polisi kinachoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kusaidia kupambana na magenge katika nchi hiyo ya Carribean yenye matatizo.
Kutokuwa na uhakika na hofu vimekuwa vikitanda tangu uamuzi wa Ijumaa, huku ghasia zikifikia rekodi mpya wakati magenge yakiimarisha udhibiti wao katika mji mkuu wa Haiti na kwingineko. Rais wa Kenya William Ruto amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Haijulikani ni muda gani hiyo inaweza kuchukua na kama nchi nyingine ambazo ziliahidi kutuma vikosi vidogo ili kuimarisha operesheni ya mataifa mengi zingezingatia kufanya hivyo pekee. Miongoni mwa waliopanga kutuma vikosi ni Bahamas, Jamaica, Belize, Burundi, Chad na Senegal.