Waziri Blinken aanza ziara ya Mashariki ya Kati

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, anaelekea Mashariki ya Kati huku kukiwa na juhudi kubwa za kidiplomasia ili kuanikisha ufikishaji  wa misaada ya kibinadamu huko Ukanda wa Gaza iliyokumbwa na vita, kukiwa na shinikizo la kimataifa kwa Israel kupunguza vifo vya raia wa Palestina.

Hii ni ziara ya nne ya Blinken, Mashariki ya Kati toka shambulizi la Oktoba 7 la Hamas dhidi ya Israel na kusababisha vita vinavyo karibia kumaliza mwezi wa tatu.

Hamas inachukuliwa kama taasisi ya kigaidi na Marekani, Uingereza, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine.

“Waziri huyo atatembelea Uturuki, Ugiriki, Jordan, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Israel, Ukingo wa Magharibi, na Misri kwa kwa mikutano na mawaziri wenzake wa mambo ya nje na wengine,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Matthew Miller, amesema Alhamisi.