Watu sita akiwemo msimamizi mkuu wa eneo moja waliuawa katika shambulizi la kuvizia na watu wenye silaha katika eneo la Abyei linalodaiwa na Sudan na Sudan Kusini, maafisa wa eneo hilo walisema.
Eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta linakabiliwa na mapigano ya mara kwa mara, ambapo makundi hasimu ya kabila la Twic Dinka kutoka Jimbo jirani la Warrap nchini Sudan Kusini, na Ngok Dinka kutoka Abyei wako kwenye mzozo kuhusu eneo la mpaka wa kiutawala.
Naibu Msimamizi Mkuu wa Abyei Noon Deng na timu yake walishambuliwa kando ya barabara kutoka Abyei kuelekea mji wa Aneet walipokuwa wakirejea kutoka kwenye ziara rasmi katika kaunti ya Rummamer, ambako walikuwa wakisherehekea Mwaka Mpya, maafisa wa serikali walisema.