Vikosi vinavyotaka kujitenga vya Tuareg, Jumatano vimetangaza kuweka vizuizi katika barabara muhimu za kaskazini mwa Mali, ambako jeshi limeingia katika njia hizo katika wiki za karibuni.
Muungano wa kudumu wa kimkakati CSP, ambao ni waasi, umesema umeamua kuweka vizuizi katika barabara zote zinazokwenda katika mpaka wa kaskazini na Maurirania, Algeria, na Niger.
Itajumuisha na barabara zinazokwenda katika miji ya Menaka, Kidai, Gao, Timbuktu, na Taoudeni, imesema taarifa ya CSP.
Taarifa hiyo imeongeza kusema kwamba vizuizi hivyo vitajumuisha njia zote za usafirishaji pia. Vikosi vikuu vya Kituareg, katika wiki za karibuni vimeshindwa katika mapambano na jeshi la Mali ambalo mwezi Novemba viliongoza kutwaliwa tena kwa mji wa Kidal.
Vita vya waasi hao na serekali vilizuka Agosti baada ya kuwepo kwa utulivu katika kipindi cha miaka minane.