Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Jumatano alipokea vyema makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku nne huko Gaza na kusema anatumai makubaliano kati ya Israel na Hamas yataimarisha juhudi za kufikia mwisho wa mzozo wao.

Ramaphosa amekuwa mmoja wa sauti maarufu katika bara la Afrika kuhusu vita vya kikatili kati ya Israel na Hamas ambavyo vimeendelea kwa takriban wiki saba.
Uungaji mkono mkubwa wa Afrika Kusini kwa Wapalestina ulianza tangu enzi za Rais wa zamani Nelson Mandela, huku nchi hiyo ikifananisha masaibu yao na hali yao kabla ya kumalizika kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994. Hata hivyo Israel inapinga ulinganisho huo.